Monday, December 22, 2008

DAMU YA YOYOTE ATAKEYEPOTEZA CHUO...IWE JUU YENU VIONGOZI WA WANAFUNZI.......!!


Mlipowataka wagome ili mtimize malengo yenu enyi DARUSO na viongozi wa wanafunzi wa SUA,MUCCOBS,ARDHI,DUCE,MUCE na DIT walifanya hivyo pasipo kujua ni nani amepanga huo mgomo.....!!
Mlipowaomba waandike mabango na wakatae kuingia darasani ili malengo ya wanaharakati feki yatimie...masikini wanafunzi waliitikia wito wenu na kuwaamini.................!!
Mlipowahamasisha waimbe kwa nguvu na wakimbie kwa nguvu na wahamasisheni...masikini wanafunzi waliitikia wito wenu na kufanya hivyo...........!!
Sasa wapo vijijini kwao na wameambiwa warudi kwa mashrti kibao...na wengine watashindwa......!!
Kibaya zaidi wale wa Ushirika wameambiwa walete na vyeti vyao vya form 4 na 6 wadahiliwe upya......................!!
Endapo mwanafunzi yeyote yule atapoteza chuo kwa upumbavu wenu viongozi wa wanafunzi........basi damu yake iwe juu yenu..........!!....Laana iwe juu yenu kwasababu sasa wapo kwenye matatizo mpo kimya na hamuwasaidii chochote...ila wao waliwasaidia kutimiza malengo yenu..........!!
HEBU NENDENI KANISANI MTUBU MAKOSA YENU NA MUMUOMBE MUNGU ASIPOTEE HATA MWANAFUNZI MMOJA..SABABU LAANA ITAKUWA JUU YENU!!

6 comments:

Anonymous said...

hey kila mtu kaburi lake,
wanafunzi wote wana akili timamu so kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe,

weye ukiambiwa ingia kisimani utaingia tu bila kupima? eti kasema kiongozi,

viongozi wana makosa na wanafunzi walokubali ndio hasa wenye makosa kwani wao wasingefanya mgomo hao viongoızi peke yao wasingefua dafu..

hakuna mtoto mchanga apo kazi kwenu ndio watajifunza sku ya pili

Anonymous said...

Ni kweli hakuna mtoto mdogo Vyuo vikuu lkn vipi linapokuja suala la kushinikizana na kupigana mawe punde baadhi ya watu wanapoonyesha kutotaka kuunga mkono mgomo fulani?
Mimi nafikiri wanaotakiwa kulaaniwa zaidi ni viongozi ksbb wao ndo ma'organizer wa kila kitu na walaaniwe zaidi(walaaniwe square) wale wa vyuo vingine vyote MUCE,DUCE,SUA,MUCCOBS,DIT na takataka nyingine kwa kitendo chao cha kuwaiga sehemu ya Mlimani,nyie ni watu wazima moreover mpo Vyuo vikuu kila mtu anaamini mpo safi kiakili lkn mmeshindwa kabisa kuthibitisha hilo,mnaigaiga tu...mmeona wenzenu wamegoma na nyie mnagoma,mlipoulizwa eti "Solidarity" solidarity? pelekeni basi hiyo solidarity yenu kwa zile familia ambazo sasa hivi zina struggle huku na kule kutaka kukamilisha taratibu za kurudi vyuoni kwa watoto wao,mbona mmekaa kimya.
Mnaiga tu,mtakuja kuiga vitu visivyoigwa siku 1,shauri yenu.

Anonymous said...

Nimeona na kushiriki migomo chuo kikuu. Mingine tuliikubali na mingine tuliipiga chini tukaendelea na madarasa. Lakini hay ya siku hizi ya kugoma na kuchukua masnap kama mamodo wa migomo inaonekana vijana wa siku hizi hawajui wanafanya nini. Kama ningekuwa mkuu wa chuo watu wote waliotokea kwenye hizo snap wasingerudi chuo kirahisi maanake ushahidi ninao kama wao ndio vinara wa migomo.
Najua kuna tatizo hapo la serikali, uongozi wa chuo na serikali za wanafunzi, lakini approach ilotumika is a total failure. Nafikiri itakuwa fundisho kwa vizazi vya sasa hivi.

Anonymous said...

We bwana kwenye mgomo force ya mob mbaya unaweza kufa kwa kupigwa kiberiti na petroli.

Bora ugome ulinde maisha yako, woote tunajuwa ukiwa traitor unapata nini!! Subirini migomo/miziro mengine yako hata huko mtaani yaja mfano:
1. mtu asipokuja harusini nyie hamwendi kilioni kwake akifiwa.
2.asiposalimia hamnunui dukani kwake hata kama mna shida ya bidhaa.
3. Hamli kwenye sherehe yake kwa sababu eti kaonekana mara kadhaa hali katika sherehe kadhaa.

Na mengine mengi, so migomo (social pressure) ni culture ya watanzania.

Anonymous said...

kama hutaki kugoma funga virago vyako mapema ondoka chuoni,
usikae maeneo hayo,ukikaa kweli utapigwa mawe na petrol,
nenda sehemu yoyote mbali na hapo mpaka wano maguvu wakimaliza utarudi,
na kama kila mtu akiondoka na hao viongozi ,mamodo whatever u call them comes hawataona watu na watagoma peke yao na hapo serikali itajua wawashike nani.

ni my views tu!

Anonymous said...

Migomo iliyo effective huwezi kukacha maana haiwezekani watu woote wakache, itakamata kama 80% hivi. Na hiyo 20% iliyobaki itaipata. Amabo huwa wana jeuri ya kupinga kugoma ni wale wanafunzi ambao ni askari, maana mkiwauwa, kabla hamjaondoka, vifaru vimeshawazunguka.