Saalam Wadau,
Ninaomba kulileta hili swala nikiwa na masikitiko makubwa sana.
Ninadhani wanafunzi wengi wengi waliingia kwenye migomo bila kufahamu ni nini impact ya migomo au bila kufahamu nini wanachodai au bila kufahamu kama maombi yao yatakubaliwa au lah....!!
Lakini vile vile nadhani walikuwa wamekosa meditation ya kujua ni njia nyingine ipi wanayoweza kutumia ili kufikisha madai yao!!
Ninasema hivyo kwa sababu mnamo leo asubuhi nilipita chuo kikuu cha Dar Es Salaam na kuona wanafunzi wengi sana wakiwa wamejazana internet cafe ya hall one kuchukua form za kuikubali sera ya kuchangia elimu ya juu ili warudi Chuoni...Sasa swali ni je kama waligomea sera hiyohiyo kwa nini sasa wanajaza form za kuikubali?? Je mlikuwa mnataka likizo fupi ya kukaa nyumbani au mlikuwa hamfahamu mnachodai??..mimi naona ya kwamba mmepungukiwa upeo na mmekosa meditation!!
Viongozi nyie ndio kabisa hamna kitu kwa sababu mliwekwa madarakani kusaidia wanafunzi,lakini sasa msaada wenu uko wapi endapo matatizo mliyotakiwa kuyashughulikia kisomi na kwa busara mnayaleta kwa wanafunzi wayashughulikie kwa njia ya migomo.......mmekosa meditation na nyie..hamfai kuitwa viongozi wa wanafunzi bali ni viongozi wa migomo.....nikiwa nimefocus moja kwa moja kwa DARUSO na wengine kwa sababu hamna mlichowasaidia wanafunzi mpaka sasa zaidi ya kuwa mmewaongezea matatizo na saivi mmekaa kimya!!
wanafunzi ada walizogomea ndio hiiiizo wanalipa ??sasa mmewasaidia nini wakati saivi wanahangaika mtaani kusaka ada ili warudi chuoni..........wengine siku walipofukuzwa chuo walilala vituo vya mabasi na watoto wa kike wakalala sehemu ambazo hazielezeki na za aibu na wengine wakaanza kutafuta nauli kwa njia zisizo nzuri.....
hamna mlichotusaidia wazembe nyie,.......................................!!..na wanafunzi msishabikie tu migomo bali muwe mnawaquestion viongozi ni steps zipi wamezifuata zikashindikana ndio sasa suluhisho ni mgomo!!...........
Mwisho nimeamini kuwa baadhi yenu mlitumiwa na vyama vya siasa kuendesha migomo na mlikuwa mnalipwa kwa kila siku ya mgomo.....!!
YOU BETTER CONTROL YOUR MINDS AND MEDITATE!!