Thursday, February 19, 2009

MAVAZI YA WANAFUNZI WA VYUO!!

Nadhani wadau mlifuatilia bunge la Dodoma,

Kati ya maswali yaliyoulizwa na wabunge mojawapo ilikuwa ni mavazi ya watoto wa kike na kiume wa vyuo vya Elimu ya ju,hasa hasa walisisitiza mavazi ya watoto wa kike kuwa si ya tamaduni zetu na yamejawa vishawishi vitupu.

Naibu waziri wa Elimu mama Kabaka alijaribu kuwatetea watoto wa kike na akasisitiza hakuna aliyewahi kufeli kisa mavazi yao.....Mimi bado halijanikaa kichwani nikichukulia mfano wa vyuo vya Dar es Salaam ka mfano.Hivi ni kweli ni kitu ambacho cha kawaida kwa mtu kuvaa mavazi ambayo si muda wake au ambayo hayafai wakati wa lecture au shughuli nyingine za chuo!!

Ukirudi katika mzingira ya kawaida tunayotoka katika familia zetu za kiTZ watoto wa kike na wa kiume huvaa kwa heshima kabisa,ila tatizo hutokea pale wanapokanyaga vyuoni na ndipo vituko huanza ili waende na wakati....mimi nahisi ni balaa na kupoteza utamaduni wetu na pia kujenga picha mbaya kwa jamii!!

Mavazi mazuri kama sketi na magauni ya heshima yamekwenda wapi wadada,au ndiyo sare yenu ya vinguo vya kubana na kuvaa nusu uchi, si usomi wal si kwenda na wakati nahisi ni ulimbukeni na kukosa maadili..tabia hutabiriwa kupitia mavazi pia...hii ndio hufanya hata wazinzi wa mitaani kuhisi watoto wa kike wazuri wapo vyuoni, kumbe ni mavazi mabaya huvutia ngono na uzungu tunaouiga hauna faida!!
Chukueni hatua na badilikeni jamani,hii hufanya nyie kuuza utu wenu ili mpate vitu vya thamani na viwalo vya thamani ili mu sustain kwenye competition zenu na fashion shows zenu za vyuoni!!

14 comments:

Anonymous said...

Nyakuwa, we sasa hivi ni nusu msomi, hutakiwi kujadili mswala ya uhuru binafsi. Watu wamevaa, hawajafeli, na hawajavunja sheria yeyote.

Watu wanataka kuwa sexy, wavutie, na wanavutia hasa ndo maana watu waona UD kuna totoz. Kwani UD umeona chuo cha dini/misheni?

Halafu nyie jamaa hamtabiriki, watu wakiwa sexy mnapiga kelele, wakijihifadhi kwa ijabu kelele, mnataka nini?

Anonymous said...

Point of addition.
Kila mtu ana uhuru wa kufanya mambo yake sawa,hii ni kwa mujibu wa katiba lkn alichokizungumzia Nyakua ambacho na mimi nakiunga mkono ni kuwa hawa Ma'binti siku hizi hawavai kwa utaratibu,wanavaa-vaa tu,mavazi yana taratibu zake bwana,ni lazima mtu uvae kuendana na mazingira na shughuli unayokwenda kuifanya,utakuta Binti anaingia Class na nguo Mgongo wote uko nje,Class....saa 2:00 mpaka 10:00/10:30 unaanika Mgongo tu,hii ni nini sasa?
Wizi mtupu!

Anonymous said...

Anselm, hilo neno "lazima" inabidi ulitoe kama wewe unataka usomi. "Lazima" kwa sheria ipi tena ikiwa katiba iko kimya?

Kwa nini unataka watu wafuate "standard" zako za mavazi?

Ili mradi hamna sheria inayosema "vaa hivi" basi akina dada wako saafi kabisa.

Na hivyo unvyosema wanavaa-vaa unaonyesha we ni radical/extremist.

Anonymous said...

Sikulaumu kijana kutobadilishwa kwa mitaala toka kipindi cha mkoloni ndo madhara yake haya ya kuzalisha wasomi ambao argument zao ni za kipumbavu kabisa. Sasa msomi wa chuo kikuu unaweka mada ya kipumbavu namana hii hivi wasomaji watakuelewaje. Ni bora umgeweka mada hii na ukawa na point zinazoeleweka lakini una argue kama mtoto wa shule za msingi. Mr. Nyakua elewa yakuwa utamaduni hubadilika kutokana na wakati na mazingira hivyo usitegemee kile kilichosadikika kipindi cha ujima kiendelee kuwa hivyo hadi leo. Elewa ya kuwa fasheni ni sehemu ya utamaduni wa muda ambao huja na kuondoka. Ngoja nikupe mfano kidogo, siku za nyuma zilikuja laizoni kila mmoja alipena kuwa nayo lakini hivi sasa ni wachache sana walio nazo zimebaki kama kumbukumbu ya enzi hizo. Hivyo wewe kama msomi naomba ujenge tabia ya kujisomea mambo mbalimbali hususani Cultural Anthropology, utajifunza mengi kuhusu jamii nyingi na vitu vinavyochangia mabadiliko kwenye jamii zilizo nyingi. Naomba usiudhalilishe usomi ambao kwa hivi sasa unapondwa na watu walio wengi na kuona kwamba kwa hivi sasa elimu ya vyuo vikuu Tanzania haimsaidii mwanafunzi kuwa na uwezo wa kuchanganua mambo. Na hili laweza kujidhihirisha iwapo mtu atapita hapa na kusoma haya mawazo yako.

Anonymous said...

anony hapo juu nimekukubali mitaala yetu kwa enzi hizo ililenga kuwazalisha vibaraka wachache kwa manufaa ya wazungu. Ebu fika vyuo vikuu vyetu leo hii mtaala alioutumia JK kipindi hicho akisoma uchumi Dar hadi sasa hivi ndo huo huo unaofuatwa, yaani kukariri kwa kwenda mbele. Mitihani yote inayofanyika kwa hivi sasa inatolewa kwenye "past papers" sasa kwa hali hii unafikiri tutakuwa na wasomi wanaotumia mbongo zao kweli. Siku hizi ni kusomea mitihani tu na si ujuzi na maarifa ambavyo hujenga maana halisi ya usomi. Anyway bora liende.

Anonymous said...

Anony wa 8:47pm,hakuna cha u'radical wala extremist hapa,ninachozungumzia hapa ni uhalisia,unajua Mabinti na hata Ma'kaka wengi wa kizazi chetu hiki wamethiriwa na vi'tabia vya kuigaiga,sasa tunaiga hadi tunapitiliza,vimini vyote,pedal,migongo wazi na kila aina ya nguo za ajabuajabu zimetokea huko Mashariki/Magharibi ya mbali,sikatai mtu kwenda na fashion ya wakati huu lkn tuangalie fashion hizi tunakwendaje nazo,hata mimi ni mtu wa kwenda na fashion lkn ninajitahidi kuvaa kutokana na Mazingira,kwa mfano natamani nyinyi watu mngeniona nilivyovaa leo hapa kwa ofisi kwa wakati huu ninapowakilisha haya maoni yangu(trouse safi,shati la akili na tai ya heshima) tofauti na nilivyokuwa nimevaa juzi Jmosi usiku Makumbusho wakati nilipokuwa naruka Nzobo na matembele,huwezi kunikuta nimekuja ofisini na jeans au pensi hata siku 1,sasa kuna umuhimu gani kwa ma'binti kutuanikia migongo,mapaja au kutuonyesha mapito ya underwear zao kwa nguo zao laini wanazovaa darasani wakati wa lecture?
Sidhani kama tunahitaji sheria ituambie wakati huu vaa hivi na wakati ule utavaa vile(ofcourse kwenye baadha ya maofisi nasikia kuna rules zinazotoa muongozo wa namna hiyo) lkn sisi wenyewe tunapaswa kuangalia hizi issues kwa marefu na mapana.

Anonymous said...

Anse, una uhuru wa kuvaa utakavyo au kuvaa kama watakavyo watu unaowagwaya au unaowaiga. Hata tai, shati na suti ni za magharibi pia.

Ujue pia mavazi ya kike yako aina nyingi na wana uhuru wa kuvaa vazi lolote, saa yoyote na mahali popote, huu ni uhuru halisi wa kikatiba.

Ikiwa wataacha kutumia uhuru wao na kuvaa kama watu wengine (akina anselm) watakavyo basi wana uhuru wa kuogopa watu pia.

Ila msichana nayejiamini mwacheni atumie uhuru wake na awe accountable na mwenyewe.

bado nasema, kulazimisha watu wavae kama utakavyo ni radicalism na extremism. Hamna guideline za mavazi.

Anonymous said...

Nyie mnataka watu wavae uniform kama ST JOSEPH?

Anonymous said...

UD SIO CHUO CHA DINI

Anonymous said...

Wizi mtupu!!!. pumba tupu za wengi wa waliochangia kuunga mkono vimini na vichupi wavaavyo wana wa UDSM, kwishilia mbali maadili yetu!!!!!!
Naunga mkono mada ya mtoa hoja!!!

Anonymous said...

We jamma hapo juu kuna kitabu wapi cha maadili ya kitanzania?

Waache watu wawe huru, mavazi hayawafanyi washindwe masomo.

Pia ujue UDSM sio chuo cha dini wala hakimilikiwi na dini. Ni chuo huru cha kisekyula.

Anonymous said...

watu mna muda wa kutosha kufanya vituko! yaani haya mambo ya kujadili fulani kavaaje hayajakwisha tu huko bongo?duh!jamani kweli kukosa historia kunamadhara yake. tatizo ni kuwa hatuna historia ya mwafrica kabla ya kuja kwa mkoloni.
lakini pia nadhani kuwa na vyou vichache na watu kukosa cha kufanya vinachangia watu kutafuta cha kusema ilimradi tu siku ipite!!
njoo huku uone wanavyuo wanavyovaa na kukumbatiana darasani kama lecturer hajaanza kufundisha,au ktk mapumziko!sasa hao wanao piga kelele si wataishia kufanya maturubai ktk suruali zao wakiona watoto walivyoweka mapaja wazi??
siwalaumu,yaacheni haya yatakwisha yenyewe,mkiyafuatilia mnayapa moto hata aliyekuwa hayaoni anafumbuka macho kutazama!praAAAAAAAAA))))))))

Unknown said...

Dress However U want but be decent

edryayagi said...

Casinos Near Carson, NV - MapyRO
Casinos Near 군포 출장안마 Carson, Nevada · 원주 출장마사지 Casinos 사천 출장샵 Near Harrah's · Casinos Near Harrah's 바카라 사이트 유니 88 · Harrah's Valley Center · Hotels Near 구리 출장안마 Harrah's · Valley Center · Funner.