Thursday, April 16, 2009

MATOKEO YA UCHAGUZI UDOM!!

(Ijumaa-Machi 27,2009) Chuo Kikuu cha DOOMA (Udom) kulikuwa na Uchaguzi Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi (UDOSO).Mchuano mkali ulikuwa ni kwa wagombea wa nafasi ya Rais wa College of Social Sciences and Humanities,nd.Ambrose Maratho na nd.Terri Gilead.

Matokeo kamili ya uchaguzi huo yalikuwa kama ifuatavyo:-Nafasi ya Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu kizima cha Dodoma (UDOSO),Raymond Magambo alishinda kwa kupata kura 2675 huku mpinzani wake David Nyangaka akiambulia kura 1076.Ngazi ya makamu wa Rais wa UDOSO ilinyakuliwa na nd.Milton Isaya kwa kupata kura 1894 huku mpinzani wake Nd.Eliphace akipata kura 1768.Ngazi ya College,matokeo yalikuwa kama ifuatavyo:- College of Social Sciences and Humanities,aliyeshinda nafasi ya Rais ni nd.Ambrose Maratho aliyepata kura 1257 huku mpinzani wake Nd.Terri Gilead akiambulia kura 790.Nafasi ya Naibu Rais ilichukuliwa na kijana kutoka Zanzibar,Nd.Bakari Ali Khamis kwa jumla ya kura 1282 huku mpinzani wake Bi.Ngungi Rhoda (mwenye asili ya Kenya) akipata kura 759.College of Education,nafasi ya Urais ilinyakuliwa na Nd.Sabhuni Joel kwa kupata kura 905 huku wapinzani wake Nd.Johannes Paul akipata kura 325 na aliyefuatia ni Dunia Salutwe aliyepata kura 200.Nafasi ya Makamu ilinyakuliwa na Bi.Ndelwa Uria na kumshinda vikali mpinzani wake Nd.Msilanga Miyango.

College of Informatics (wazee wa Computer) hakukuwa na upinzani,kwani kila nafasi ilikuwa na mgombea mmoja mmoja tu.Nafasi ya Rais ni Nd.Honorious Amon na Makamu wake ni James Chambo.

(April 3,2009) siku ya ijumaa,viongozi hao wapya wameapishwa na mwanasheria na kamishna wa viapo,akishuhudia makamu mkuu wa Chuo kikuu cha Dodoma (UDO) ,Prof.Idriss kikula na kupewa ridhaa ya kuanza majukumu yao hayo mazito ya kuwatumikia wanachuo wenzao.
SELEMANI TAMBWEBA.PSPA 2nd Year

1 comment:

Anonymous said...

Jihadhari kutaja ukabila na utaifa wa mtu au udini. Kawaida vitu hivi si utambulisho wa uanafunzi bora au uongozi bora.

Umetaja mzamzibar na mkenya, mbona hao wengine hukutaja kama ni wa iringa na rukwa sijui?

Au unahisi tanganyika ndo wenyewe na wengine ni wakuletwa? Kwani wewe ni afisa uhamiaji?

Siku nyingine utaje kabila, dini na mkoa uliotoka kabla hujataja vya wengine.